Home EDUCATION MAWAIDHA | Faida za kufungua mwezi mtukufu wa ramadhan

MAWAIDHA | Faida za kufungua mwezi mtukufu wa ramadhan

Mawaidha | Faida za kufunga mwezi mtukufu wa ramadhan

DARSA NO. 1

NI ZIPI FADHLA ZA KUFUNGA SAUM SIKU MOJA KWA AJILI YA ALLAH SUBHANA WA TA’ALA?

Anasimulia Abu Said (Radhwiya Allahu Anhu) kwamba Rasul ﺻﻠﻰ
ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ alisema:
“Mtu yeyote afungae
Saumu SIKU MOJA ktk njia Ya Allah Subhana Wa Ta’ala, kwa sababu ya siku hiyo Moja, Allah
Subhana Wa Ta’ala
Atauweka USO wa Mtu huyu mbali na MOTO wa
JAHANNAM kwa umbali
sawa na mwendo wa
MIAKA SABINI”.
Imepokelewa Na
(Bukhari na Muslim).

Allahu Akbar… Ndugu zangu ktk emaan hiyo ndio fadhla ya kufunga Saum siku moja tu kwa ajili ya Allah Subhana Wa Ta’ala. Jee tukikamilisha Mwezi mzima tutapata Fadhla kiasi gani? Namuomba Allah Subhana Wa Ta’ala Atujaalie kuifunga Ramadhan Kwa Amani Na salama na In shaa Allah tuzipate Fadhla Hizi nyingi. Tuwakumbukeni ktk dua NDUGU zetu wa Palestine Allah Subhana Wa Ta’ala Awasahalishie na Awafanyie wepesi ktk mtihani huu mzito uliowakumba. Allahuma ameen.

Kupata Elimu Zaidi endelea kufuatilia website yetu ya www.minambaxelamedia.com look

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here